TIMU za Uingereza zina nafasi ya kuandika historia kwa kuwa ligi ya kwanza Ulaya kuingiza vilabu vinne kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa na Europa.
Liverpool na Tottenham Hotspur bado ziko kwenye ligi ya mabingwa, wakati Alhamisi hii Arsenal na Chelsea zinacheza na Valencia na Eintracht Frankfurt kwenye nusu fainali za ligi ya Europa.
Arsenal wamepoteza michezo mitatu mfululizo kwenye ligi ya Uingereza – kipigo cha mwisho wakikipata dhidi ya Leicester kwa mabao 3-0 walipotembelea dimba la King Power. Kipigo hicho kimefifisha matumaini ya Arsenal kumaliza katika nafasi nne za juu ili kuweza kushiriki ligi ya Mabingwa Ulaya.
Matumaini yao ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao ni kushinda Europa pekee. Wanacheza dhidi ya Valencia dimbani Emirates katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali huku Valencia wakiwa katika nafasi ya uhakika kushiriki lii ya mabingwa msimu ujao.
Kocha wa Arsenal Unai Emery alisema walijisikia vibaya kupoteza dhidi ya Crystal Palace, Wolves na Leiceste City “Lakini tunahitaji kuendelea. Tuna ligi mbili ambazo bado tunahitajika kucheza vizuri ligi ya Uingereza na Europa. Zote hizi zina nafasi ya kutufikisha kwenye ligi ya mabingwa ambalo ndio lengo letu.
“Tunatakiwa kuendele kuwa imara kiakili na kujiamini kwamba tunaweza,” alisema.
Chelsea ni timu ambayo imenufaika na kiwango kibovu cha Arsenal, hivyo wameweza kujiimarisha katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi – wao watacheza dhidi ya Eiintracht Frankurt.
Timu hiyo kutoka ligi ya Bundesliga sio ya kupuuzwa, ushindi wao dhidi ya Inter Milan na Benfica kwenye hatua zilizopita inaonyesha jinsi gani walivyo wazuri. Ikiwa ndiyo timu pekee kutoka Bundelsiga katika mashindano ya Ulaya, matumaini yote ya Ujerumani yapo mabegani mwao hivyo Chelsea watakuwa na kazi ya ziada kuwatoa.
Chesea wanacheza mchezo huu baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United Jumapili iliyopita. Eden Hazard anasema yeye pamoja na wachezaji wenzake wataingia katika mchezo huo wakiwa na kujiamini zaidi baada ya mchezo wa Man United.
“Ilikuwa ni vizuri (sare dhidi ya United) ila tungeweza kufanya vizuri zaidi” alisema baada ya mchezo. “Sare sio matokeo mabaya kwetu nadhani kama tungejiamini zaidi tungepata bao jingine na kushinda mchezo”
Mechi hizi zitaonyeshwa kupitia StarTimes pekee. Arsenal vs Valencia utakuwa LIVE kupoitia ST World Football saa 4:00 Usiku na Eintracht Frankfurt vs Chelsea LIVE kupitia ST Sports Premium saa 4:00 Usiku. Kwa wateja wa Antenna ni kifurushi cha UHURU kwa Tsh 18000 tu na wateja wa Dish ni kifurushi cha SMART kwa Tsh 21,000.

from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2VJBxDS
No comments:
Post a Comment