Saturday, 4 May 2019

ORIGI AIFUNGIA LIVERPOOL DAKIKA ZA MWISHONI YAILAZA NEWCASTLE UNITED 3-2

Mshambuliaji Mbelgiji mwenye asili ya Kenya, Divock Origi akiifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya 86 ikiwalaza wenyeji, Newcastle United 3-2 usiku huu Uwanja wa St. James' Park, Newcastle. Origi alifunga bao hilo dakika 13 tu tangu aingie kuchukua nafasu ya Mmisri, Mohamed Salah na mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na beki Mholanzi, Virgil Van Dijk dakika ya 13 na Salah dakika ya 28, wakati ya Newcastle yalifungwa na Christian Atsu dakika ya 20 na Solomon Rondón dakika ya 54.
Kwa ushindi huo, Liverpool inarejea kileleni ikifikisha pointi 94 baada ya kucheza mechi 37, sasa ikiizidi tena Manchester City pointi mbili, ambayo hata hivyo mchezo mmoja mkononi 


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2H25wPe

No comments:

Post a Comment

Vaal Best Bets Thursday 9 May 2019

Winning Form brings you their best tips for Vaal's racing on  Thursday, 9 May 2019 . Comments and betting and silks are provided! Tips p...