Saturday, 4 May 2019

NI WYDAD NA ESPERANCE FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA 2019

FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2019 itazikutanisha timu za Kaskazini mwa Afrika tupu mwishoni mwa mwezi huu, mabingwa watetezi, Esperance ya Tunisia wakimenyana na Wydad Casablanca ya Morocco.
Hiyo ni baada ya timu hizo kuzitoa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini baada ya mechi za marudiano leo ugenini.
Esperance imelazimisha sare na TP Mazembe Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi ikitoka kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Tunisia, wakati Wydad nayo imetoka 0-0 na Mamelodi ikitoka kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza Morocco.

Zilikuwa mechi nzuri za Nusu Fainali leo, ikishuhudiwa wageni wote wakicheza michezo ya kufanana ugenini, kujihami kulinda ushindi wa nyumbani.
Na sasa wababe hao wa Kaskaini mwa Afrika watakutana katika fainali, mechi ya kwanza ikifanyika Mei 24 Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat, Morocco na marudiano Mei 31 Uwanja wa Olimpiki mjini Rades, Tunisia.


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2GU3y2k

No comments:

Post a Comment

Vaal Best Bets Thursday 9 May 2019

Winning Form brings you their best tips for Vaal's racing on  Thursday, 9 May 2019 . Comments and betting and silks are provided! Tips p...