Thursday, 2 May 2019

LACAZETTE AFUNGA MAWILI ARSENAL YAICHAPA VALENCIA 3-1 EUROPA LEAGUE

Mshambuliaji Mfaransa, Alexandre Lacazette akishangilia baada ya kuifungia Arsenal mabao mawili dakika za 18 na 25 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Valencia kwenye mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Emirates mjini London. Bao la tatu la Arsenal lilifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 90, wakati la Valencia lilifungwa na Mouctar Diakhaby dakika ya 11 na timu hizo zitarudiana Mei 9 Uwanja wa Mestalla mjini Valencia na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Chelsea na Eintracht Frankfurt kwenye fainali Mei 29 


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2GYwxDp

No comments:

Post a Comment

Vaal Best Bets Thursday 9 May 2019

Winning Form brings you their best tips for Vaal's racing on  Thursday, 9 May 2019 . Comments and betting and silks are provided! Tips p...