Mshambuliaji Gonzalo Higuain anayecheza kwa mkopo kutoka Juventus akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la tatu dakika ya 75 ikiilaza 3-0 Watford kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge mjini London. Mabao mengine ya Chelsea yamefungwa na Ruben Loftus-Cheek dakika ya 48 na David Luiz dakika ya 51 na kwa ushindi huo The Blues inafikisha pointi 71 baada ya kucheza mechi 37 na kujihakikishia kumaliza ndani ya nafasi nne za juu hivyo kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao PICHA ZAIDI GONGA HAPA
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2WkGlNf
No comments:
Post a Comment