Saturday, 27 April 2019

MSUVA APIGA ZOTE MBILI DIFAA HASSAN EL-JADIDI YAICHAPA MOGHREB TETOUAN 2-0 MOROCCO

Na Mwandishi Wetu, CASABLANCA
WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefunga mabao yote mawili timu yake, Difaa Hassan El-Jadidi ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Moghreb Tetouan katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan.
Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga SC ya Dar es Salaam alifunga mabao yake hayo dakika za 63 na 73 na kuwapa raha mashabiki wa timu hiyo inayotumia jezi za rangi ya kijani na nyeupe.
Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El –Jadidi inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 26 na kupanda hadi nafasi ya tano kutoka ya nane kwenye msimamo wa Botola Pro inayoshirikisha timu 16.
Simon Msuva (kulia) akishangilia baada ya kufunga mabao yote mawili Difaa Hassan El-Jadidi ikishinda 2-0 dhidi ya Moghreb Tetouan 

Vigogo Wydad Casablanca waliopo Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ndio wanaongoza ligi hiyo kwa pointi zao 53 za mechi 25, wakifuatiwa na Raja Casablanca wenye pointi 47 za mechi 25 pia.
Kikosi cha Difaa Hassan El –Jadidi kilikuwa; Mohammed El Yousfi, Youssef Aguerdoum, Marouane Hadhoudhi, Ayoub Benchchaoui, Ettayb Boukhriss, Mohammed Ali Bemammer, Bakary N’diaye, El Mehdi Karnass/Chouaib El Maftoul dk72, El Mostafa Chichane, Bilal El Magri/Sekou Camara dk55 na Simon Msuva/Adil El Hasnaoui dk87. 
Wakati huo huo: Naye Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu klabu yake, JS Saoura jana ilishinda 3-1 dhidi ya CS Constantine katika mchezo wa Ligi Kuu ya Algeria Uwanja wa Agosti 20, 1955 mjini Bechar.


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2vrxrBG

No comments:

Post a Comment

Vaal Best Bets Thursday 9 May 2019

Winning Form brings you their best tips for Vaal's racing on  Thursday, 9 May 2019 . Comments and betting and silks are provided! Tips p...